Waliketi Chini Lyrics – Katani West Church Choir Lyrics

Waliketi Chini Lyrics Video - Katani West Church Choir Lyrics

STANZA 1
Waliketi chini kwa fikara wakawaza
je tuzidi dumu kwa ukame Bethlehemu
au tutoke jawabu tuendeni Moabu
je ni kitu kipi ni cha faida huku
chakula kweli duni hawana subira
ya kustahimili magumu.

CHORUS:
Na wakaandamana kwenda familia ya Elimeleki
hawakujua kwamba heri kufa njaa
nyumbani Bethlehemu kwenye Mungu yuko
wakapiga hatua moja hatua mbili
mbele mbele hadi ugenini
ni dhahiri kuwa Moabu si nyumbani kwetu.

Watch Waliketi Chini Lyrics Video Here

FOLLOW OUR WHATSAPP CHANNEL FOR MORE UPDATES

STANZA 2
Tabia na hulka zile za kibinadamu
hatuchunguzi uvumi wa kushiba kwao
wale wa Moabu piga hesabu mara mbili
tutaweza imbaje wimbo wa kifalme
kule ugenini haiwezekani
Bethlehemu mimi sitoki

CHORUS:
Na wakaandamana kwenda familia ya Elimeleki
hawakujua kwamba heri kufa njaa
nyumbani Bethlehemu kwenye Mungu yuko
wakapiga hatua moja hatua mbili
mbele mbele hadi ugenini
ni dhahiri kuwa Moabu si nyumbani kwetu.

FOLLOW OUR WHATSAPP CHANNEL FOR MORE UPDATES

SHARE THIS POST