Bwana Nimerudi Tena Lyrics- Praise Team T.A.G Forest Ya Kwanza Lyrics

Bwana Nimerudi Tena Lyrics- Praise Team T.A.G Forest Ya Kwanza Lyrics

Bwana nimerudi tena
Yesu nakushukuru
wengine sijui
ila mimi Bwana
nimejua umenitendea
Bwana nimerudi tena
Yesu nakushukuru
mengine sijui
ila hili Bwana
nimejua umenitendea X5

Nimeomba mengi
umenijibu moja
umetutendea wengi
mimi nimerudi
japo mengine bado
ila natambua
thamani ya hili moja
ulilolitenda
wale wengine kenda mimi sijui
ila nachojua kwangu umetenda
mengine sijui
ila hili Bwana
nimejua umenitendea

Watch Bwana Nimerudi Tena Lyrics Video Here

Mimi ni Msamaria tu
mtu wa makabila mengine
wala sikustahili haya
uliyonitendea
wengine sijui wanaona nini
ila mimi Bwana
ninauona wema huu wa ajabu

Wenye ukoma tulikuwako
na neno lako
halikufanya makosa
wengine sijui
ila mimi Bwana
nimejua umenitendea

Wenye dhambi tulikuwa wengi
na damu yako ikanitakasa
wengine sijui
ila mimi Bwana
nimejua umenitendea

Utukufu kwako tu
na Heshima zote
(kwako tu)
Umenitenda wema
Umenitenda vyema
Umenitendea wema mkuu X4

Umenitenda wema
Umenitenda vyema
Umenitendea wema mkuu X4

FOLLOW OUR WHATSAPP CHANNEL FOR MORE UPDATES

SHARE THIS POST